May 23, 2019

IMEELEZWA kuwa nyota 12 wa kikosi cha kwanza ndani ya Simba wamekalia kuti kavu ambapo kwenye ripoti iliyokabidhiwa kwenye uongozi wa Simba hatma yao ya kuongeza mkataba inategemea sauti ya Patrick Aussems ambaye ni kocha mkuu wa Yanga.

Nyota hao ni pamoja na Adam Salamba, Rashid Juma, Asante Kwasi, Juuko Murshid, Nicholaus Gyan, Zana Coulibary, Mohamed Ibrahim, Yusuph Mlipili, Pascal Wawa na Paul Bukaba.

Habari za ndani zimeeleza kuwa nyota hao wamegawanywa kwenye makundi mawili ambapo kundi la kwanza ni la wale ambao watatolewa kwa mkopo ili kukuza viwango na kundi la pili ni wale ambao watapewa mkono wa kwa heri.

Nyota ambao inaaminika watatolewa kwa mkopo ni pamoja na Adam Salamba ambaye msimu huu haukuwa bora kwakwe amepachika mabao matano pekee, Rashid Juma ambaye bado hajakomaa licha ya kupewa nafasi, Yusuph Mlipili, Paul Bukaba na Juuko Murshid.

Wale ambao inaamanika kocha bado hajawaelewa ni pamoja na Kwasi, Coulibary, Mo Ibrah, Gyan na Wawa.

Wengine ambao tayari wametolewa kwa mkopo ni pamoja na Marcel Kaheza ambaye yupo nchini Kenya na Mohamed Rashid anayekipiga KMC.

Aussems amesema kuwa anachoamini yeye wachezaji wake ni bora na wafanya kile ambacho anawaambia isipokuwa wapo wale chipukizi ambao hawaonyeshi uwezo mkubwa.

"Kwenye kikosi changu nimekuwa nikiwabadilisha ili kujua uwezo wao, ila wote wana uwezo mkubwa isipokuwa baadhi wanashindwa kuonyesha kile ambacho wanacho," amesema.

3 COMMENTS:

  1. Mwandishi wa story hii anaipenda kweli Yanga, mpaka anasema Patrick Aussems ni kocha mkuu wa Yanga!Kuweni makini kwy proof-reading jamani. Makosa kama haya yanaonyesha kama hampo serious na kazi yenu!

    ReplyDelete
  2. IMEELEZWA kuwa nyota 12 wa kikosi cha kwanza ndani ya Simba wamekalia kuti kavu ambapo kwenye ripoti iliyokabidhiwa kwenye uongozi wa Simba hatma yao ya kuongeza mkataba inategemea sauti ya Patrick Aussems ambaye ni kocha mkuu wa Yanga....duh, rekebisha hapo mkuu wetu

    ReplyDelete
  3. aliyekabidhi hiyo ripoti ni nan? maana ripot imekabidhiwa kwenye uongozi na nan halafu sauti ambayoinasubiriwa ni ya kocha Patrick aliyekabidhi ripot ni nan? maana kama ni kocha tayari angekabidhi ripot ya uhakika kuwa hawa siwahitaji sasa hapo nan kakabidhi ni manara au ni nan SALEH mbona mwajichanganya kaka humu kuna watu siyo mbumbu kama taarifa haijakamilika si uiche kwanza au unataka upande wa pili waanze mchecheto kuwa wachezaji wameechwa kumbe ndo bado hata kikao cha bodi na benchi la ufundi wewe waleta taarifa subir kijana mda upo tu.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic