May 23, 2019


Imeelezwa kuwa Mshambuliaji wa Yanga, Amiss Tambwe amesema kuwa hajui hatma yake ndani ya klabu hiyo.

Taarifa zinasme kwamba Tambwe ameeleza kuwa  mwenye maamuzi pekee ya kumua aendelee kubaki ama aondoke ni kocha wake Mwinyi Zahera.

Adha, taarifa hiyo imesema Tambwe amedai atajua hatma yake mwisho wa msimu huu kama anabaki Yanga au anaondoka.

Pia imeelezwa kuwa Tambwe amesema mpaka sasa ana ofa tatu mezani ambapo mojainatoka kwao Burundi na nyingine Zambia na moja ni ya hapa hapa Tanzania.

Licha ya uwepo wa ofa hizo, Tambwe amesema bado anawapa Yanga kipaumbele cha kwanza kabla ya kufanya maamuzi mengine kwenda sehemu nyingine.

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic