May 7, 2019


MENEJA wa Manchester City, Pep Guardiola amesema kuwa alimzuia nahodha wa kikosi hicho, Vincent Kompany kupiga shuti ambalo lilileta bao la ushindi mbele ya Leicester City
Ushindi huo umeirejesha City kileleni baada ya kufikisha jumla ya pointi 95 na kuishusha Liverpool yenye pointi 94  ikiwa nafasi ya pili, kama watashinda mbele ya Brighton Jumapili basi watatwaa kombe lao msimu huu la Ligi Kuu ya England.
"Nilimwambia Kompany, hapana usipige shuti, usipige shuti ukiwa nje ya 18," amesema Guardiola.
Kompany alipuuzia sauti ya bosi wake huyo na kuachia shuti akiwa nje ya 18 ambalo lilizama nyavuni, na hili ni bao lake la kwanza akiwa nje ya 18 baada ya kupita miaka 11. 
"Niliskia sauti ikinizuia kupiga shuti, usipige shuti, usipige shuti ndivyo nilivyoskia ila nikaiambia nafsi yangu, sikuwa na namna zaidi ya kufanya kile ambacho nilikifanya wakati nikiwa bado kijana sana," amesema. 

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic