HAWA NDIYO WANAOTAJWA KUONDOKA SIMBA, UONGOZI WAJA NA TAMKO ZITO. MIKATABA YATAJWA
Wachezaji hao wote hivi sasa wanaruhusiwa kufanya mazungumzo na klabu nyingine watakazomuhitaji kwa mujibu wa kanuni za Fifa ambazo zinamruhusu anapobakiza miezi sita katika mkataba wake ambao wao wamebakisha mwezi mmoja pekee.
Mwenyekiti wa timu hiyo, Swedy Mkwabi alisema kuwa hivi sasa wanachokifanya ni kukisuka kikosi chao kwa ajili ya msimu ujao kwa kuhakikisha wanakuwa na wachezaji wenye sifa na uwezo wa kucheza michuano ya kimataifa.
Mkwabi alisema, kamwe hawatakubali kumuachia mchezaji yeyote anayehitajika kubaki Simba baada ya kupokea mapendekezo ya kocha mkuu wa timu hiyo Mbelgiji, Patrick Aussems. Aliongeza kuwa, wachezaji hao wanaotajwa kuondoka Simba Niyonzima, Okwi na Mkude wote wapo kwenye mipango ya kocha huyo, hivyo wapo tayari kuwabakisha kwa dau lolote Simba.
“Simba tunachokifanya hivi sasa ni kuziboresha baadhi ya sehemu zenye upungufu kwa kusajili wachezaji wenye uwezo mkubwa na uzoefu wa kucheza michuano mikubwa ya kimataifa.
“Hivyo ni ngumu kwetu kuwaachia wachezaji kama Okwi, Niyonzima na Mkude wote wenye sifa zinazohitajika ndani ya Simba, kikubwa tunachokifanya ni kuziboresha baadhi ya sehemu zenye upungufu kwa kusajili wachezaji wapya wazuri zaidi ya hao tuliokuwa nao kwa lengo la kuongeza changamoto ya ushindani.
“Wapo baadhi watakaoachwa kwa mujibu wa mapendekezo ya kocha lakini siyo hao wanaotajwa, malengo yetu Simba tunaangalia kimataifa zaidi baada ya mwaka huu kuondolewa hatua ya Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika,” alisema Mkwabi ambaye ni muwekezaji mkubwa mjini Tanga.
0 COMMENTS:
Post a Comment