May 18, 2019


Kuelekea mchezo wao na Simba, Kocha wa Ndanda, Khalid Adam amefunguka kuwa wanahitaji pointi mbili kuwa na uhakika wa kubaki ligi kuu kwa msimu ujao, hivyo Simba wajipange tu.

Simba inatarajiwa kuvaana na Ndanda kesho Jumapili kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam baada ya
awali kukutana kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona na kutoa sare.

Kocha huyo alisema tayari kikosi chake kipo Dar na kinaendelea na maandalizi na lengo ni kupata ushindi na kuwa kwenye nafasi nzuri.

Ndanda kwa sasa ina pointi 47, huku wapinzani wao Simba wakiwa na pointi 85 na wanahitaji pointi nne pekee kuweza kutangaza ubingwa.

“Tupo Dar na tunaendelea na maandalizi yetu na tunahitaji pointi mbili kujihakikishia kutoshuka daraja.

“Mechi yetu na Simba siyo rahisi, tumejipanga kuona tunaondoka na pointi tatu muhimu, najua wapinzani nao wanasaka ushindi kuona wanatetea ubingwa wao msimu huu. Hivyo tumejipanga na hatuhitaji kupoteza na wachezaji wote wako fi ti kabisa bila shida,” alisema Adam

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic