May 1, 2019

KOCHA Mkuu wa JKT Tanzania, Mohamed Abdallah 'Bares' amesema kuwa alijipanga kupata sare kwenye mchezo wa jana kupoteza kwa kufungwa bao 1-0 uwanja wa Uhuru kumevuruga hesabu zake.

Bares amesema kuwa aliitambua Simba mapema namna inavyocheza hasa kwa kutumia viungo wao na washambuliaji wengi ambao wana uchu wa kufunga muda wote hali iliyomfanya aingie kwa kujilinda na kushambulia kwa kushtukiza.

Akizungumza na Saleh Jembe, Bares amesema alitumia muda mwingi kusoma mbinu za wapinzani wake hali iliyomfanya aanze kwa kujilinda na kushambulia kwa kushtukiza.

"Simba ina timu nzuri na kubwa hasa ukizingatia imetoka kushiriki michuano ya kimataifa, wachezaji wake wana uzoefu tofauti kidogo na wangu hilo nililitambua ndio maana nikaongeza nguvu kujilinda na kushambulia kwa kushtukiza.

"Kufungwa kwetu kumeniumiza pia hata kutolewa kwa mchezaji wangu Anuary Kilemile kuliongeza ugumu wa mchezo ila hakuna namna tutaendelea kupambana kwenye michezo yetu inayofuata," amesema Bares.

JKT Tanzania ipo nafasi ya 13 kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara baada ya kucheza michezo 33 imejikusanyia pointi 39 kibindoni.

4 COMMENTS:

  1. JKT walicheza vizuri ila referee kama alikuwa akiogopa kuwaadhibu JKT kwani walicheza foul nyingi na za wazi la kushangaza refa alikuwa hachukui hatua yeyote hata ile foul aliofanyiwa Chama ni foul ya wazi kabisa lakini refa kapeta labda alihofu kuambiwa anaipendelea Simba kama angetoa foul nyingi kwa JKT.

    ReplyDelete
  2. Mashabiki Yanga wameshatia sumu mbaya sana ya kuwa Simba inabebwa na hivyo marefarii wamekuwa wanachezesha mechi za Simba na timu pinzani wakiwa na mchecheto.Ukitaka ukweli nenda kwenye Azam TV ktk kipindi cha "kipyenga chetu" kinachoendeshwa na marefarii wastaafu wenye beji za FIFA ndipo hapo utabaini mbivu na mbichi.Sielewi kwa nini mtu ulalamike kuongezwa muda wakati ni sheria kama kuna timu inapoteza muda kwa makusudi na isitoshe muda si unaongezwa kwa timu zote mbili?

    ReplyDelete
  3. Kweli kabisa kuna faulo kama mbili ambazo ni dhahiri shahiri VAR ingeamua penalty itokee!

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic