May 1, 2019


MRISHO Ngassa, mshambuliaji wa Yanga, amefuta ndoto za Azam FC kuwania ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu huu kutokana na bao lake alilofunga dakika ya 13 kuongeza pointi kwa Yanga na kuwaacha wapinzani wao mikono mitupu.

Mchezo wa Azam FC na Yanga uliochezwa uwanja wa Uhuru ulikuwa na ushindani mkubwa huku Azam FC wakitumia nguvu nyingi kusaka ushindi ila juhudi zao zilikwama baada ya kushindwa kupata bao kwenye mchezo huo uliochezwa.

Akizungumza na Saleh Jembe, Kocha Meja Msataafu, Abdul Mingange amesema kuwa timu yake kwa sasa imepoteza matumaini ya kutwaa ubingwa msimu huu.

"Kwa sasa hatuna matumaini ya kutwaa ubingwa tena hasa ukiangalia idadi za mechi ambazo tumebakiwa nazo pamoja na utofauti wa pointi na timu nyingine bado inakuwa ngumu kwetu kutwaa ubingwa msimu huu.

"Kwa jinsi Yanga na Simba zilivyo itakuwa ngumu kwao kupoteza michezo yote waliyobakiwa nayo ila licha bado tuna nafasi ya kupambana kwa mechi ambazo zimebaki kushinda mechi zetu zote," amesema.

Azam FC ipo nafasi ya tatu baada ya kucheza michezo 33 imejikusanyia pointi 66 huku kinara Yanga anapointi 77 wote wamebakiza michezo mitano na Simba yenye pointi 69 imebakiwa na michezo 10 ikiwa nafasi ya pili.

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic