May 7, 2019


Baada ya kupokea kipigo cha mabao 2-0 dhidi ya Lipuli katika mchezo wa Kombe la FA, Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera amesema walikuwa na malengo ya kumaliza ligi katika nafasi ya tano au sita.

Kauli ya Zahera imekuja mara baada ya kuona ndoto hizo zinaenda mkono wa kushoto kulingana na namna mwenendo wa ligi ulivyo hivi sasa.

Zahera amefunguka hayo akiwa amepoteza malengo mawili mpaka sasa ikiwemo taji la SportPesa na Kombe la Shirikisho ambayo aliahidi kuwa wanaweza wakachukua.

Mbali na mataji hayo, Zahera pia aliahidi kutwaa taji la ligi lakini kwa namna msimamo ulivyo hivi sasa katika Ligi Kuu Bara uhakika wa kutwaa taji hilo haupo kutokana na watani zao wa jadi Simba kuwa vizuri zaidi.

Baada ya kupoteza mchezo wa jana, kikosi cha Yanga kinatarajia kusafiri kuelekea Mara kwa ajili ya mechi na Biashara United ambayo ni ya ligi itakayopigwa kwenye Uwanja wa Karume.

13 COMMENTS:

  1. Yanga fanyeni hima huyu Kocha atawaliza sana...huzuni na simanzi zitaendelea sana mtaendelea kubagazwa na kutaniwa mtaani kwa muda sana ikiwa malengo hayakuwa kuchukua ubingwa mlikuwa mnashindana na kushinda mechi kwa nia gani? Sidhani ni majibu mazuri kutoa kwa mwalimu wa mpira miguu aliyebobea....kwamba kwa timu yenye historia na ukubwa kama wa Yanga kushiriki ligi na kulenga kuwa ya 6, 7 au 8 katika msimamo wa ligi.....haya ni malengo ya JKT, Kagera, Singida United, Alliance nk. Si kwa timu kubwa kama Yanga kujiwekea malengo kama haya!

    ReplyDelete
  2. Zahera Hajawahi Kuishiwa Alisema Lipuli Iliwafungaga Yanga Kwakuwa Hakuwepo Jana Alikuwepo Kipigo Ndo Kikaongezeka, Akasema Atachukua Mataji Ma Tatu Sportpesa, FA Na Ligi kuu Kwa Sasa Anasema Hakutegemea Kushika Nafasi Ya Pili Huyo Kocha Ni Muongo Tena Mwana Siasa Mkubwa Kocha Wa Simba Ni Mwana Sayansi Yy Anadili Na Vitendo Tu

    ReplyDelete
  3. Kutokana na kauli za Zahera za sasahivi ni zakuvunja moyo zaoneshsa hakuna tanaa ya lolote na kanyanyua mikono juu ni kuwa mbio za sakafuni huishia ukingoni. Namnasihi asivunjike moyo. Falling down is not a defeat, but a defeat is to remain where you have fallen.

    ReplyDelete
  4. Niliwahi kusema zahera bahati yake yupo ndani ya yanga inayopitia kipindi kigumu, kabla ya kupokwa ubingwa na simba, yanga imechukua ubingwa mara tatu mfululizo halafu leo mtu anasema ana malengo ya kumaliza nafasi ya sita au saba kama kapanda daraji juzi vile. Tunapotoa maoni watani mnatuona kama tunawakejeli lakini hapo kocha hamna.

    ReplyDelete
  5. hakuna kocha hapa .ile mechi ya prisons dsm baada ya mechi kocha wa prisons richard aDOLF aliongea vizuri sana kuwa huyo zahera hajui kitu kuhusu soka yeye amekalia kuzungumzia vitu ambavyo vipo nje ya soka

    ReplyDelete
  6. wana yanga tuamke tusimpe madaraka makubwa huyu kocha zahera as if yeye ndiye kaanzisha yanga hakuna kocha hapa tumfukuze makocha wapo wazuri sana kama kocha wa kmc hivi unaanzaje kuizungumzia simba wakati jahazi linazama huku yanga?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Khaa! kwanza hii kauli yake imenishangaza sana. Hivi huyu ni Kocha Proffessional au ndo anajifunza ukocha!

      Au inawezekana alipokuwa anakuja huku kuifundisha Yanga alijua kuwa anakuja kufundisha timu ambayo ndio kwanza imepanda daraja kama KMC au BIASHARA UTD?

      Lakini nazidi kupata nae mashaka zaidi kutokana na namna anavyopingana na kauli Zake. Alitamka yeye mwenyewe kwamba atachukua, Kombe la Sports Pesa (Akachemka mapemaaa), akasema kuwa atachukua kombe la FA (huko ndio kabisaaaaa, Kapigwa kipigo cha mbwa mwizi / kipigi cha aibu) yule mbwa waliyemuulizia siku walipomfunga Prison, badala ya wao kumla, mbwa huyo kawala wenyewe hadi kichwa. Bado Zahera akasema kuwa wanashindana na Simba kutwaa Ubingwa wa Bara, kwa madai kwamba Azam sio washindani wao tena. Leo anasema kuwa walipanga kushika nafasi ya 5 au 6!.

      Anataka kuiga mipango ya Simba kusema kuwa walipanga kufika makundi Ligi mabingwa lakini wamefika Robo, kwahiyo Simba ikaonekana kuwa imevuka malengo. Hivyo, nae anatafuta sasa sifa ya kuambiwa kavuka malengo!. Hapo ndugu zangu wana-Yanga mnachezewa akili tu, AMKENI. Kwa Kocha huyo nafasi za juu mtakuwa mnazisikia tu kwa wenzenu. Mtabaki kuwapa lawama bureeee waamuzi na TFF, kumbe uozo mnao wenyewe ndani.

      Delete
  7. Zahera kalewa sifa kafanywa kuwa ni muokozi na akajaaliwa yeye ndie kila kitu na bila ya yeye Hakuna modern yanga. Alianza kuiandama Simba na
    Manara wake kuwa inapendelewa na ushindi wake kuwahonga marefa na hata katika uchaguzi akitajwa yeye ndio rejea la kusisimuwa. Kamdhalilisha Kakolanya na kila MTU akafunga mdomo Kwa kudai Haki yake na huku akiwafumbia macho wengine waliokuwa wakigoma usiku na mchana

    ReplyDelete
  8. Najiuliza hivi kwa nn Zahera alimpanga Dante na kumuacha Yondani? kwa mechi kama hii ya mtoano kweli huyu ni kocha au alichukulia lipuli kama timu ya kawaida au alijua hii ni ligi?. NILIWAHI Kusema zahera kachukua yanga kama familia yake anachokitaka anakifanya sasa yanga haiko hivyo Zahera, mheshimiwa Magu aliwahi kusema watanzania sio wajinga kuwa hawaoni sasa hapo utaipandika kauli zako leo unazipangua zote zahera kweli yanga inawachezaji wakubwa kuliko lipuli sasa nini kilichosababisha unasema yanga iwe ya saba au sita? kweli mpaka kagera mtibwa, lipuli, kmc , biashara nazo zinatushinda? ili sisi tuwe wa saba kweli?. Hapa hakuna kitu sasa maandalizi ya bilioni 3 yatatoka wapi kama haushiriki michuano ya kimataifa? hapo tumepugi mapeeeeeeeema ZAHERA OUT UTATUJUA SISI NDO WATANZANIA MWAMBIE MAXMO na ulizia soka lipoje TENA wewe hujatupa chochote kweli umenikeeera sana, kumbe ndo maana ulimweka yondani benchi ili tupigwe uendelee kutukuzwa kwa msimu mwingine umepugi me

    ReplyDelete
    Replies
    1. Duuuh! Jamaa kalalamika hdi huruma!. Si ndio huyu ambaye mlimpa jina "Bonge la Kocha". Leo hii imekuwaje tena!. Huyu ni mwanasisa nyie, mlikuwa hamjui! Hiyo kauli aliyoitoa, usidhani kaitoa tu, keshaona mbali, sasa hapo ndo kaanza kucheza na akili za uongozi mpya wa Yanga.

      Delete
  9. Kamanda wa jeshi akienda vitani hawezi kuwaambia askari wake kuwa wanaenda kuchezea kichapo na kukatwa vichwa,ni lazima awape ujasiri wa kupambana hadi tone la mwisho la damu.Mmemsahau Al saaf wa Iraq!!!!

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic