May 7, 2019


Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera, amesema malengo yao msimu huu hayakuwa kushiriki michuano ya kimataifa na hata kufika nusu fainali ya Kombe la Shirikisho.

Kauli hii imekuja mara baada ya kipigo cha jana dhidi ya Lipuli katika mchezo wa Kombe la FA

Zahera amedai hata kwenye ligi malengo yao hayakuwa kubeba ubingwa lakini baada ya kuwa wanacheza na wanashinda wakaamini kuwa wanaweza kubeba ubingwa.

Zahera ameongeza kuwa hawana cha kupoteza kipindi hiki na sasa wanajipanga kwa msimu ujao baada ya kushindwa kuwa mabingwa wa kombe na ASFC.

Na kuhusu Ligi Kuu, Zahera amesema wana nafasi dogo sana ya kuwa mabingwa kutokana na klabu ya Simba kubakiza mechi nyingi zaidi yao.

1 COMMENTS:

  1. Yanga fanyeni hima huyu Kocha atawaliza sana...huzuni na simanzi zitaendelea sana mtaendelea kubagazwa na kutaniwa mtaani kwa muda sana ikiwa malengo hayakuwa kuchukua ubingwa mlikuwa mnashindana na kushinda mechi kwa nia gani? Sidhani ni majibu mazuri kutoa kwa mwalimu wa mpira miguu aliyebobea....kwamba kwa timu yenye historia na ukubwa kama wa Yanga kushiriki ligi na kulenga kuwa ya 6, 7 au 8 katika msimamo wa ligi.....haya ni malengo ya JKT, Kagera, Singida United, Alliance nk. Si kwa timu kubwa kama Yanga kujiwekea malengo kama haya!

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic