SADIO Mane na Pierre Aubameyang washambuliaji wa timu mbili tofauti wote kwenye michezo yao ya mwisho walifunga mabao mawili na kufaya washinde kiatu cha dhahabu pamoja na Mohamed Salah.
Aubameyang alipachika mabao mawili wakati timu yake ikiibuka na ushindi wa mabao 3-1 mbele ya Burney hivyo alijiunga na Salah wa Liverpool pamoja na mchezaji mwenzake Mane ambaye alifunga mabao 2 mbele ya Wolves na kufanya wote wafikishe jumla ya mabao 22.
Pia msimu wa mwaka 2010-11, ilitokea hali kama hii ambapo Dimitar Berbatov na Carlos Teves walishinda kiatu cha dhahabu baada ya kufunga mabao 20 kila mmoja.
Mshambuliaji wa timu ya Taifa ya Gabon Aubameyang ambaye alifunga mabao mawili amesema kuwa " Nimeshinda na wenzangu wawili naona fahari kubwa sana, ni wachezaji wakubwa na wote tunatoka Afrika, ni wachezaji wakubwa kutoka Afrika tunaiwakilisha Afrika hii inapendeza.
"Ninafuraha kushinda, na ninafuraha kuwa na wenzangu, najua wachezaji wenzangu wanajua kuhusu kiatu hiki, nimewaambia hamna kitu, sihitaji kuona wote wanacheza na kuanza kufikiria kiatu nataka tucheze tukiwa ni timu nami pia ni mchezaji," amesema.
Jurgen Klopp meneja wa Liverpool amesema kuwa anamtambua Aubameyang ambaye alikuwa mchezaji mzuri.
"Auba pia? Kwa hiyo kuna viatu vitatu vya dhahabu? Ni jambo jema. Wote ni wachezaji wangu," amesema.
Salah,mwenye miaka 26, alifunga mabao 32 msimu uliopita na alitwaa kiatu cha dhahabu hii kwake ni rekodi nzuri kutwaa tena msimu huu.
Mshambuliaji wa Tottenham's Harry Kane, alikuwa mchezaji wa mwisho kubeba tuzo hiyo mfululizo ambapo alifanya hivyo msimu wa mwaka 2015-16 msimu huu ametupia mabao 17 kutokana na kusumbuliwa na majeruhi
0 COMMENTS:
Post a Comment