MSHAMBULIAJI wa zamani wa timu ya Taifa ya England, Alan Shearer amesema kuwa kiungo mshambuliaji wa timu ya Manchester United, Paul Pogba hajahusika kwenye mabao 2-0 ambayo walifungwa kwenye mchezo wao wa mwisho dhidi ya Cardiff City.
United imemaliza msimu huu ikiwa nafasi ya sita na imetofautiana pointi 32 na Manchester City ambao ni mabingwa msimu huu na imepishana pointi tano na timu iliyo kwenye nne bora.
"Baada ya msimu huu anaweza kuondoka, najua itakuwa ngumu kwake," amesema Shearer.
Pogba ndiye kinara wa upachikaji mabao ndani ya United ambapo ametupia jumla ya mabao 16 na ametoa pasi 11 ila alishindwa kuonyesha makeke yake mbele ya Cardiff' Jumapili.
Baada ya United kushinda mbele ya Paris St-Germain kwa mabao 3-1 Marchi 6 walifanikiwa kushinda kwenye mechi mbili tu kati ya 12 ambazo walicheza.
0 COMMENTS:
Post a Comment