May 18, 2019

UONGOZI wa Singida United umesema kuwa utaanza kuuza mapema tiketi wa ajili ya mchezo wao wa Mei 22 dhidi ya Simba utakaochezwa uwanja wa Namfua ambao utawakutanisha washambuliaji makini Habibu Kiyombo wa Singida na Meddie Kagere wa Simba.

Singida United iliyo chini ya Felix Minziro itamenyana na Simba ikiwa na kumbukumbu ya kupoteza kwa kufungwa mabao 3-0 uwanja wa Taifa mchezo wa kwanza.

Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Singida United Cales Katemana amesema kuwa wamejipanga vema kwa ajili ya mchezo wao hivyo wataanza kuuza tiketi mapema ili kupunguza usumbufu.


"Unajua mechi ya Simba na Singida ni kubwa na itakuwa na ushindani hivyo ili kupunguza usumbufu tutaanza kuuza tiketi Jumatatu asubuhi na bei ya kawaida ni 5,000 na viti maalumu ni 10,000, hivyo tunawaomba mashabiki wajitokeze kwa wingi" amesema Catemana.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic