UONGOZI wa Azam FC umesema kuwa kwa sasa hauna hesabu ya kutwaa ubingwa wala nafasi ya pili kutokana na hesabu kuwakataa hivyo watakomaa kwenye mechi zao mbili zilizobaki kujiandaa na mchezo wao wa fainali ya kombe la Shirikisho dhidi ya Lipuli
.
Azam FC imebakiwa na michezo miwili ambayo ni dhidi ya Mtibwa Sugar na Yanga ili kukamilisha msimu.
Akizungumza na Championi Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Azam FC, Jaffar Maganga amesema kuwa msimu uliopita walimaliza wakiwa nafasi ya pili ila msimu huu wamenyoosha mikono na kuishia nafasi ya tatu.
"Kwa sasa hatuwezi tena kutwaa ubingwa hivyo tunawaachia vigogo ambao wapo nafasi ya kwanza na ya pili ili kutwaa ubingwa huo, ila michezo yetu miwili iliyobaki tumejipanga kushinda ili kutwaa pointi tatu muhimu.
"Imani yetu ni kwamba tukifanya vizuri michezo yetu iliyobaki tunajiweka kwenye nafasi nzuri ya kutwaa ubingwa wa kombe la FA tutakayocheza na Lipuli, Juni Mosi," amesema Maganga.
Mchezo huo utachezwa uwanja wa Ilulu mkoani Lindi na bingwa wa michuano hiyo atawakilisha nchi kwenye michuano ya kimataifa ya kombe la Shirikisho Afrika.
0 COMMENTS:
Post a Comment