May 3, 2019


Imeripotiwa kwamba mechi ya Singida United dhidi ya Simba SC inayopaswa kuchezwa Mei 22 kwenye Uwanja wa Namfua katika mechi ya Ligi Kuu Bara huenda ikaahirishwa.

Taarifa zinasema mechi hiyo haitachezwa ili kupisha mechi ya kirafiki dhidi ya Sevilla itakayopigwa Uwanja wa Mkapa Mei 23, 2019.

Mchezo wa Simba na Singida sasa utabidi kupangiwa tena tarehe nyingine lakini ukichezwa kwenye Uwanja uleule wa Namfua.

Hivi sasa tayari kikosi cha Simba kipo jijini Mbeya kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Prisons unaopigwa leo saa 10 jioni.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic