May 3, 2019


KUFUATIA Mabadiliko ya uendeshaji yaliyofanywa ndani ya Simba, kupitia mfumo wa uendeshaji kuwa kwenye mfumo wa kampuni ambayo inaongozwa na mwekezaji Mohamed Dewji 'Mo', mgombea wa Yanga Magege Chotta amesema atatumia njia hiyo kuibadili klabu hiyo kulitimiza wazo hilo waliloanza kuliasisi.

Chotta ambaye ni miongoni mwa wagombea wa nafasi ya Makamu Mwenyekiti amesema anaamini kupitia mfumo wa uwekezaji bora na klabu kuwa mikononi mwa wanachama kutasaidia kuboresha uendeshaji ndani ya Yanga.

"Nina maisha kabla ya Yanga, nagombea kwa ajili ya kuisaidia Yanga ili iweze kusimama yenyewe kama yenyewe kwa kuanzisha kampuni kama ilivyo kwa Simba.

"Mfumo tulionao kwa sasa unachochea migogoro tofauti na tukiingia kwenye mfumo wa kampuni ambapo mwanachama atakuwa hana nafasi ya kuingilia utaratibu kwa kuwa vitu vyote vinafanywa na bodi ya wakurugenzi.

"Mimi ni Mkurugenzi wa Chotta Agre Enterprises Limited ambayo inajishughulisha na masuala ya kilimo hivyo sina shida ya kupigania uongozi kwa ajili ya maslahi yangu binafsi kwani nina shughuli zangu nyingine ninazofanya," amesema Chotta.

Yanga itafanya uchaguzi wake Mei 5 mwaka huu, viongozi wao watadumu kwa muda wa miaka minne kwa nafasi za Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti na Wajumbe wa Kamati ya Utendaji.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic