May 21, 2019


Kitendo cha straika wa Yanga, Heritier Makambo kusaini mkataba wa awali na Horoya AC, kimeifanya Simba kukosa kiasi cha dola laki tatu (Sh milioni 689) ambazo wangezipata kwa straika wao Meddie Kagere.

Kabla ya kusajiliwa kwa Makambo na Horoya AC ya Guinea, klabu hiyo ilishaweka mezani kiasi cha dola laki tatu kwa ajili ya kumng’oa Simba na Kumpeleka kwenye kikosi chao kwa msimu ujao.

Meneja wa Kagere, Patrick Aussems Ameliambia Championi Jumatatu, kwamba kabla ya Makambo kusaini mkataba huo, kocha wa kikosi hicho, Didie Gomes alimpigia simu kwa ajili ya kumtaka ampeleke mmoja kati ya mastraika wake Kagere au Jacques Tuyisenge wa Gor Mahia.

“Kabla ya Makambo kusajiliwa Horoya, kocha wao alinipigia simu kwa ajili ya kutaka nimpelekee kati ya Kagere au Tuyisenge na alikuwa tayari ametenga dola laki tatu (milioni 689) kwa ajili ya kumsajili mmoja wao.

“Lakini nikamwambia kwanza aanze na Makambo kwani kwa washambuliaji hao ingekuwa ngumu kidogo, lakini hata hivyo bado anataka washambuliaji wengine wawili na ninaweza kumpelekea baadaye, itategemea na namna nitakavyoelewana na timu zinazowamiliki wachezaji hawa kwa sasa,” alisema Gakumba.

7 COMMENTS:

  1. Meneja/wakala wa Kagere sio Patrick Aussems!Mwisho ndio unamtaja Gakumba, ambaye ndio jina sahihi. Jamani kuweni makini, kwani tovuti yenu haina proof-readers? Mkichanganya vitu namna hii mnaonekana hampo serious na kazi yenu!

    ReplyDelete
  2. Kagere katulia Simba na anskipata kila akitakacho kutoka Kwa bilionea Moo kijana asiyeweza kuyumbishwak

    ReplyDelete
  3. Watu wanatunga uongo mpaka wanajikanyaga wanashindwa kujua hata wakala wa mchezaji ni nani. Hii bongo watu wana lana sana kha!

    ReplyDelete
  4. Habari ya uongo na hakuna dola laki tatu zilizotolewa! Yule mchezaji kauzwa kwa hela ya vitumbua!

    ReplyDelete
  5. Sawa za vitumbua, so anaenda Guinea? au anaenda Simba

    ReplyDelete
  6. Tutamkumbuka sana Makambovichi ndani ya masimu mmoja to kafanya mambo makubwa

    ReplyDelete
  7. Uongozi mpya yaani umekuja na nuksi....wale Wanayanga wenye hasira wako wapi? Habari zinaendelea kuwa si nzuri sana wachezaji wote tegemeo wanaondoka wengine wakiuzwa na wengine mikataba ikiisha bila kuongezwa....jamani jamani hebu harakisheni kuokoa hali.....maumivu yanaendelea....hakuna habari njema wiki hizi mbili na mwezi mzima wa 5. Rekebisheni hali kwa kusajili at least mikataba ya awali ili kutoa moyo na kutia hamasa kwa wapenzi kuendelea kuchangia.....ukimya huu unaogopesha na ni hatari....mmeshaijenga chuki kwa wanayanga kuna wadau wa Yanga hawajitokezi kusaidia kwa kuwa tu hakuna dalili za kuanza kuleta mashine za uhakika hakuna hata mikataba ya awali kwa washambuliaji wakali na viungo wakali au mabeki wakali....Kuna kundi kubwa limeandaa fujo hawa ni wanachama ambao hawapendi hizi habari za huzuni zinazoendelea (Ajibu anaondoka burr, Makambo anauzwa, wachezaji 7 wanaumwa kuikosa Mbeya City, ubingwa kuchukuliwa na Simba, Sportspesa kuileta Sevila kucheza na Simba na siyo Yanga...nk. Na habari mbaya ndio zinazoendelea) Sasa amani ya nchi itavurugika....kwa kuwa kuna watu wanaumizwa na hizi habari...

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic