May 21, 2019


MWEKEZAJI wa Simba, bilionea, Mohamed Dewji ‘Mo’ ameahidi kuwapa bonsai ya shilingi milioni tano wachezaji wa timu hiyo wagawane kwa kila mechi watakayoshinda kati ya mechi nne walizobakiza, ikiwemo ya jana dhidi ya Ndanda.

Mo alitangaza neema hiyo, Ijumaa iliyopita mara baada ya kukutana na wachezaji, Benchi la Ufundi la timu hiyo na kula futari kwa pamoja kwenye moja ya hoteli kubwa jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa taarifa ambazo limezipata Championi Jumatatu, wachezaji hao watapewa bonsai hiyo kwenye michezo minne waliyoibakisha ya ligi ukiwemo wa jana walipocheza dhidi ya Ndanda FC.

Mo ameongeza dau hilo, ukiachana na Sh 400,000 ambazo amekuwa akitoa kwa kila mchezaji kila wanaposhinda, tangu ligi imeanza.

Mtoa taarifa huyo alisema, Mo amewaongezea bonasi hiyo kwa ajili ya kuwaongezea morali na hamasa ili wafanikishe malengo ya kutwaa ubingwa.

4 COMMENTS:

  1. Milion 5 kila mechi inatosha nn?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Milion tano kwa dk 90 sio mchezo wewe, uliza ni timu gani inaweza toa hio hela kwa dk 90. Safi sana Mo

      Delete
  2. Halafu eti Yanga wanasema wamefanya mazungumzo na nyota WA Simba kutaka kuwasajili Hahaaa

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kwani unaambiwa kila mchezaji atabaki simba msimu ujao,.hiyo nimeambiwa ni bonasi baba sio usajiri. Wenzako wana negotiate contract wanaweka na bonasi ndani.

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic