May 5, 2019


KIKOSI cha Manchester United leo kimejitoa kwenye timu ambazo zitatinga kwenye nne bora baada ya kulazimisha sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Huddersfield mchezo uliochezwa uwanja wa John Smith's.

Manchester United walianza kufunga bao la kuongoza dakika ya 8 kupitia kwa MC Tominay bao ambalo lilidumu kwa muda wa dakika 58 kabla ya Isaac Mbenza kusawazisha bao hilo dakika ya 60.

United imeshindwa kupata matokeo katika mchezo wa leo licha ya kutangulia kupata bao lao la kuongoza mapema.Pia kwa kushindwa kufika kwenye nne bora wanashindwa kufuzu michuano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao.

Matokeo haya yanaiacha Manchester United nafasi ya sita wakiwa wamejikusanyia pointi 66 baada ya kucheza michezo 37.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic