MAPYA YAIBUKA JUU YA CHIRWA NA AZAM, HAWAELEWANI
UONGOZI wa Azam FC umesema kuwa bado haujaelewa mshambuliaji wao Obrey Chirwa nini anakitaka kwa sasa kutokana na kutowapa jibu lolote juu ya kuongeza kwake mkataba ndani ya Azam FC.
Chirwa alisajiliwa na Azam FC msimu huu kwa mkataba wa mwaka mmoja ambapo mkataba wake unamalizika ligi itakapoisha.
Akizungumza na Spoti Xtra, Mratibu wa Azam FC, Philip Alando alisema kuwa mpaka sasa bado wapo kwenye mazungumzo na Chirwa ili aongeze mkataba ndani ya Azam FC.
“Unapomzungumzia mchezaji kama Chirwa kwetu sisi tayari ameshaingia kwenye mfumo wetu, sasa tunaendelea na mazungumzo naye ili kuona namna gani ataendelea kuitumika timu yetu ingawa hatujaļ¬ kia muafaka mzuri.
“Tunajua yeye ni mchezaji na ana maamuzi yake ila kama hatakuwa tayari kuituikia timu yetu tunamruhusu aondoke kwa kuwa kuna timu ambazo huenda anahitaji kwenda kuzitumikia,” alisema Alando ambaye ni mchezaji wa zamani wa Kagera Sugar.
Mwacheni aende zake akaendelee na kilimo cha mahindi kwao
ReplyDelete