May 3, 2019


KIUNGO mnyumbulifu wa Simba, Clatous Chama raia wa Zambia ameweka wazi kwamba licha ya kuendelea kupambana kwenye ligi lakini anasubiri kwa hamu mechi yao ya kirafi ki dhidi ya Sevilla ya Hispania.

Simba imepangwa kucheza na Sevilla katika mechi ya kirafi ki itakayopigwa jijini Dar, Mei 23
mwaka huu.

Sevilla wataletwa Tanzania na Kampuni ya SportPesa. Kiungo huyo anayevaa jezi namba 27 amesema kwamba wanaendelea na harakati zao za kutafuta matokeo kwenye kila mechi yao ya ligi lakini pia wanatumia kujiandaa na mechi hiyo na Sevilla.

“Tunaendelea kutafuta pointi katika kila mechi yetu tunayocheza. Tunapambana kwa nguvu zetu ili tufanikishe malengo ya kushinda katika mchezo huo.

“Lakini muda huohuo pia ninasubiri kwa hamu mechi yetu ya kirafi ki ambayo tutacheza hapa nyumbani na Sevilla. Ninajiandaa kwa ajili ya mechi hiyo,” alisema Chama.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic