May 23, 2019


KOCHA Mkuu wa Simba, Patrick Aussems amevuka vikwazo vyake vyote viwili alivyowekewa kwenye mkataba wake wakati anakabidiwa kikosi kwa mikakati mikali.

Simba walimpa mitego miwili Aussems ili kuona kama anaweza kuitegua kabala ya kuongezewa mkataba wake mwingine ndani ya kikosi hicho.

Lengo la kwanza ilikuwa ni kuhakikisha wanatinga hatua ya Makundi kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika ambapo walifika hatua ya robo fainali na kutolewa na TP Mazembe.

Pia jambo jingine ambalo aliwekewa ni lile la kutetea ubingwa wa Ligi Kuu Bara jambo ambalo amelitimiza pia.

Aussems ametwaa kombe la ligi akiwa amebakiwa na michezo miwili mkononi jambo ambalo amesema ni hatua kubwa kufikia kwa timu ya Afrika Mashariki.

 Kwa sasa mabsi wa Simba wanapiga hesabu za kumuongezea mkataba mpya kocha huyo raia wa Ubelgiji.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic