May 23, 2019

KOCHA wa Azam FC, Idd Cheche amesema kuwa hakukuwa na namna yoyote kwa kikosi chake jana zaidi ya kulipa kisasi kwa Mtibwa Sugar ambao walianza kuwatibulia rekodi zao kwa kuwafunga msimu huu.

Mtibwa Sugar ilikuwa timu ya kwanza kubeba pointi tatu mbele ya Azam FC mchezo uliochezwa uwanja wa Manungu kwa ushindi wa mabao 2-0.

Akizungumza na Saleh Jembe, Cheche amesema kuwa walikuwa na hasira baada ya kufungwa hali iliyowafanya wakae chini kupitia makosa waliyoyafanya.

"Kama timu ilitufunga kwenye mchezo wa kwanza hakukuwa na namna nyingine zaidi ya kuiheshimu na kuangalia pale tulipokesa ili tupate matokeo.

"Mwisho wa siku nasi pia tunahitaji pointi tatu licha ya kwamba hatupo kwenye nafasi ya pili basi hapa tulipo lazima tujishikilie," amesema Cheche.

Mabao ya Azam FC yalipachikwa kimiani na Donald Ngoma dakika ya pili na Enock Atta dakika ya 68 na kuifanya Azam FC ifikishe jumla ya pointi 72 ikiwa nafasi ya tatu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic