Huenda mwaka ukawa umeanza vibaya kwa staa wa muziki wa R&B,
Ciara baada ya kufanya vibaya kwenye mauzo ya albamu yake kwa kuambulia
kuuza kopi 100 tu hadi sasa.
Hivi karibuni, Ciara aliachia albamu yake ya saba, Beauty Marks
lakini ndani ya wiki chache ilikuwa imeuza nakala 100 ambazo ni za chini
kuliko hadhi yake na haijawahi kumtokea hali hiyo.
Licha ya kutoa nyimbo tano kutoka katika albamu hiyo ambazo ni Level
Up, Freak Me, Dose, Greatest Love na Thinkin Bout You ambazo zimekimbiza
kinoma lakini albamu hiyo imeshindwa kuuza wala kuingia hata kwenye
chati mojawapo kubwa duniani.
Hili ni pigo kwa Ciara ambaye tangu aanze muziki hajawahi kukutana na hali kama hiyo.
Alipoanza rasmi muziki mwaka 2004 aliachia albamu yake ya kwanza
iitwayo Goodies ambapo kwa wiki ya kwanza tu alivunja rekodi ya kuuza
nakala zaidi ya 124,000.
0 COMMENTS:
Post a Comment