May 2, 2019


MSEMAJI wa Familia ya Dkt, Reginald Mengi ambaye alikuwa ni Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Michael Ngalo amesema kuwa utaratibu wa msiba wa Mengi utatolewa kesho baada ya kukamilisha taratibu na watu waliopo Dubai.

Ngalo amesema kuwa ni pigo kubwa kwa Taifa kiujumla ila mipango ya Mungu huwezi kuzuia na kuwashukuru Watanzania kujitokeza kwenye msiba huo.

"Tunawashukuru Watanzania wote kwa kujitoa kwenye msiba huu, ila hamna namna kazi ya Mungu haina makosa, utaratibu kuhusu mazishi yake utatolewa kesho kwani bado tunaendelea kufanya mawasiliano na wenzetu wa Dubai," amesema Ngalo.

Mengi amefariki Usiku wa kuamkia leo akiwa Dubai taarifa ambazo zimepokelewa kwa mshtuko mkubwa na Watanzania wengi.

Pia alikuwa ni mwanamichezo wa muda mrefu kwani alikuwa mlezi wa timu ya Serengeti Boys kabla ya kufikwa na mauti.

Pumzika kwa Amani, Dkt Mengi

4 COMMENTS:

  1. Mungu Ailaze mahali pema Roho ya marehemu Reginald Mengi

    ReplyDelete
  2. This comment has been removed by the author.

    ReplyDelete
  3. R.I.P Mzee Mengi. Wewe ulikuwa ni mfano katika maeneo mengi uliyoyasimamia. Ulikuwa rafiki pia. Siku zote tulipoonana ulinisalimia kwa kuniita '' My brother..". Ulikuwa mtu wa watu na utabakia kukumbukwa kwa mema yote uliyoyatenda duniani. Mungu akurehemu upate pumziko la milele, Amen.

    ReplyDelete
  4. Rest in peace Doctor Mengi, Amen

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic