May 2, 2019


KOCHA Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera amefunguka kuwa moja ya vitu ambavyo vinamfelisha kwenye  baadhi ya mechi na kushindwa kupata idadi kubwa ya mabao ni kutokana na kukosa mawinga wazuri ambapo anaamini kama angekuwa nao angefanya vizuri zaidi ya walivyo kwa sasa.

Kocha huyo amesema ana idadi ndogo ya wachezaji ambao wanaweza kumudu kucheza nafasi hiyo kwenye kikosi chake ambao ni Mrisho Ngassa, Deus Kaseke na Jaffary Mohammed pekee jambo ambalo linafamnya afeli iwapo anataka kushambulia kutoka pembeni.

“Kuna muda huwa nahitaji aina ya wachezaji fulani kwenye mechi lakini inakuwa shida kutokana na wachezaji ambao ninao hapa. Kama kwenye mechi na Azam FC kama ningepata mawinga wazuri basi ninaamini tungeshinda mabao 4-0 tofauti na ile 1-0 ambayo tulishinda.

“Kwa mfano wale wao walikuwa wanacheza kwa pasi sana na tukaruhusu wacheze hivyo sasa unawadhibiti kwa watu wa pembeni ambao wanaenda mbio, unapata mpira unapiga kwao, lakini ndiyo sina kwa sasa japo ninawahitaji kwenye baadhi ya mifumo ambayo ninahitaji tucheze,” alisema Zahera.

Kwa sasa Yanga inawatumia zaidi Ngassa na Kaseke kucheza kama mawinga kwenye mbalimbali za kikosi hicho.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic