May 20, 2019


MWENYEKITI wa Klabu ya Yanga, Dk Mshindo Msolla, amesema kuwa mafanikio aliyoyapata mshambuliaji wao Mkongomani, Heritier Makambo hayajatokea kwa bahati mbaya bali ni juhudi za mchezaji hivyo awe somo kwa wachezaji wengine wa kikosi hicho.

Nyota mwingine Yanga ambaye anatajwa kuweza kutimka ndani ya Yanga kutokana na kuwa na mchango mkubwa ni nahodha Ibrahim Ajibu ambaye mpaka sasa ni kinara wa kutoa pasi za mabao.

Ajibu ametoa jumla ya pasi 17 za mabao na amefunga mabao sita hali inayofanya kasi yake kuwa juu msimu huu wakati timu yake ikiwa nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi.

Makambo yeye ametupia jumla ya mabao 16 kwenye ligi akiwa nyuma ya mabao sita na kinara wa kutupia Meddie Kagere mwenye mabao 22.

Msolla amesema kuwa mafanikio ya Makambo yawe chachu kwa wachezaji wa Yanga kwani kuna timu zaidi ya nne ambazo zinawinda saini yake mbali na klabu ya Horoya AC ambapo alikwenda kufanya vipimo.


1 COMMENTS:

  1. Yanga msijidanganye nendeni kwenye mabadiliko hamuwezi kutegemea michango eti kwa kigezo kuwa mna mashabiki na wanachama milioni moja .....kwa uhalisia uchumi hauruhusu watu kuchangiachangia milele....watu wa kipato cha chini wengi wao hawana mwamko wa Kuchangia....nyie tafuteni mwekezaji kama walivyofanya Simba mambo yaende....ukiona mna ahidiahidi na michakato kuwa mingi ni dhahiri kuwa hamna fedha za kuanza vurugu za usajili

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic