May 20, 2019

BAADA ya kukubali kichapo cha mabao 2-0 mbele ya Simba, beki wa Ndanda FC, Abdallah Mfuko amesema kuwa walishindwa kuwadhibiti Simba kutokana na ubora wao pamoja na wao kushindwa kutumia nafasi ambazo walizipata.

Ushindi wa jana uwanja wa Uhuru umeifanya Simba kujikita kileleni ikiwa na pointi 88 huku Ndanda wakishuka mpaka nafasi ya nane wakiwa na pointi 47.

"Haikuwa bahati yetu, tulipambana kutafuta matokeo tukakwama, ila ukweli ni kwamba Simba ipo vizuri na ndio maana tukapoteza.

"Tumetengeneza nafasi lakini zote ziliweza kuzuiwa na wapinzani wetu, bado tunaendelea na mapambano kwa ajili ya michezo yetu iliyobaki muda bado unaruhusu makosa yetu benchi limeyaona na linafanyia kazi," amesema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic