May 23, 2019


IMEELEZWA kuwa Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera ana mkakati maalumu wa kusuka kikosi kipya cha Yanga ambacho kitakuwa na mastaa wapya baada ya wale waliopo ndani kwa sasa kusepa.

Katika kutengeneza kikosi hicho imeelezwa kuwa wachezaji 10 wanaachwa moja kwa moja ndani ya kikosi hicho ambacho kinaanza harakati za kurejesha heshima msimu ujao.

Mastaa hao ni pamoja na Amiss Tambwe, Thaban Kamusoko ambaye sababu kubwa inayotajwa ni umri kwenda, Juma Mahadhi, Athony Matheo, Baruhani Akilimali ambaye anasumbuliwa na majeruhi, Ibrahim Hamid kipa namba tatu ambaye Zahera hajui alisajiliwa na nani.

Pia yumo Said Makapu, Deus Kaseke, Klaus Kindoki ambaye bado Zahera anaendelea kumwamini ndani ya kikosi, Mrisho Ngassa.

 Zahera amesema kuwa mpango mkubwa msimu ujoa ni kuwa na kikosi imara ambacho kitashindana na timu yoyote na kitapata matokeo chanya na wachezaji wote atawatangaza Mei 28.

1 COMMENTS:

  1. Usitangaze uamuzi WA kufukuza wachezaji bila ya kuhakikisha hela ya wachezaji wapya umezitia mkononi. Ikiwa upo juu ya MTU usiwache Tawi kabla ya kukamata Tawi jengine

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic