May 23, 2019


BAADA ya wachezaji wa kikosi cha Singida United kukubali kufungwa mabao 2-0 na Simba juzi uwanja wa Namfua uongozi wa Singida United umesema kuwa wamepishana na mamilioni ambayo yalitengwa kwa ajili ya ushindi wao.

Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Singida United, Cales Katemana amesema kuwa waliwaambia wachezaji wao kwamba endapo watashinda kila mmoja angepata kiasi cha shilingi laki mbili na viongozi wa mkoa waliongeza dau kufikia milioni kwa atakayefunga bao.

"Haikuwa bahati yetu na wachezaji wetu walipambana wameshindwa hivyo wamepishana na fedha ambazo zilikuwa zimetengwa kwa ajili yao kwani mbali na milioni sita ambazo zilitengwa na timu viongozi na wadau waliweka mezani milioni moja kwa kila bao.

"Kila kitu kilikuwa wazi maana mchezo wa mpira haufichiki, hivyo hamna namna nyingine wachezaji wamekosa milioni kwa kuwa hakuna aliyefunga, kasi yetu tunailekeza kwenye mchezo wetu wa mwisho dhidi ya Coastal Union utakaochezwa mkoani Tanga," amesema Katemana.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic