KOCHA msaidizi wa Tanzania Prisons, Shaban Kazumba amesema kuwa walishindwa kupata matokeo jana baada ya kuzidiwa ujanja na viungo wa Yanga mchezo uliochezwa uwanja wa Uhuru.
Kazumba amesema kuwa walipambana kupata matokeo ila haikuwa bahati yao baada ya kubwana mbavu na wapinzani wao Yanga.
"Tulipambana na tulijipanga kupata matokeo ila tulizidiwa katikati na viungo wa Yanga hali iliyofanya tushindwe kupata pointi tatu kwenye mchezo wetu," amesema Kazumba.
Tanzania Prisons wamefungwa na Yanga nje ndani kwani mchezo wa kwanza walifungwa mabao 3-1 uwanja wa Sokoine na jana walifungwa mabao 2-1 uwanja wa Uhuru.
0 COMMENTS:
Post a Comment