BREAKING: BASI LA TANZANIA PRISONS LAPATWA NA AJALI KIBAMBA DAR ES SALAAM
Basi walilokuwa wamepanda wachezaji wa Prisons iliyocheza na Yanga kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar limepatWa ajali.
Kwa mujibu wa nahodha wa timu hiyo, Elibarik Fadhil, amesema wakati wakiwa maeneo ya Kibamba waligongwa nyuma na gari la mafuta huku vioo vya gari vikipasuka na kupoteza baadhi ya vitu ikiwa ni majira ya saa nne usiku.
Imeelezwa kuwa Polisi walifika eneo la tukio na kuchukua data za tukio hilo na mpango wa kubadilisha gari ulianza kufanyika ili safari iendelee.
Imeelezwa pia hakuna mchezaji aliyefariki zaidi ya majeraha kwa baadhi ya wachezaji
0 COMMENTS:
Post a Comment