May 5, 2019


SIMBA Leo wametwaa pointi tatu uwanja wa Sokoine na kufanikisha kujinyakulia pointi sita katika uwanja huo na jumla ya mabao matatu huku wao wakifungwa bao moja pekee.

Walianza juzi kwa kufuga mabao 2-1 mbele ya Mbeya City kabla ya leo kubeba pointi tatu leo mbele ya Prisons kwa ushindi wa bao 1-0.

Bao la ushindi leo limefungwa na mshambuliaji Emmanuel Okwi dakika ya 11 akimalizia pasi ya James Kotei lililodumu mpaka dakika ya 90 mchezo wa leo.

Ushindi huo unaifanya Simba kufikisha jumla ya pointi 78 ikiwa nafasi ya pili baada ya kucheza michezo 30, wanabakiza pointi mbili kuifikia Yanga ambayo ina pointi 80 ikiwa nafasi ya kwanza.

Yanga imecheza michezo 34 na imejikusanyia pointi 80 tofauti ya michezo minne na Simba ambao wamebakiza michezo minne ili kuwa sawa na Yanga.

Mchezo unaofuata kwa Simba ni Mei 8 dhidi ya Coastal Union utakaochezwa uwanja wa Taifa.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic