UONGOZI wa Simba umesema kuwa iwe jua ama mvua ubingwa unarejea mitaa ya Kariakoo kutokana na ubora wa kikosi na morali waliyonayo wachezaji wa Simba kwa sasa.
Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa kwa sasa mechi zao zote zilizobaki wanabadilisha mbinu na kucheza zaidi ya fainali kwani wanahitaji ubingwa.
"Hakuna ambacho kwa sasa Simba inahitaji zaidi ya ubingwa na ndio maana mfumo unabadilika kwa mechi zetu za mwisho, tunaanza kucheza kwa mtindo wa kimataifa.
"Wachezaji wanajua umuhimu wa kushiriki michuano ya kimataifa kama Ligi ya Mabingwa Afrika sasa hawawezi kufika huko kama hawatabeba kombe, hivyo hesabu ni kombe mengine yatafuata," amesema Manara.
Simba ni kinara wa ligi kwa sasa akiwa na pointi 88 anahitaji pointi moja ili kutwaa ubingwa msimu huu.

Kwahivo ikiwa ni hivo basi 99.99% ubingwa ni wetu sisi Wanasimba
ReplyDeleteIkiwa ni hivo basi 99.99% ubingwa ni wetu sisi Wana Simba
ReplyDelete