KOCHA wa timu ya Lipuli, Seleman Matola amesema kuwa timu yake kwa sasa inapitia kipindi kigumu kutokana na gharama za uendeshaji kuwa kubwa na fedha hakuna.
Akizungumza na Saleh Jembe, Matola amesema kuwa kwa sasa hali ya kikosi sio shwari kiuchumi kutokana na gharama za kuendesha kuwa kubwa.
"Timu ina mchezo Mei 22 ambapo tutacheza na Ndanda, mkoani Mtwara, mpaka sasa hatujajua ni namna gani tunaweza kwenda kwani hakuna fedha za kutupeleka huko na hata tukipata kwa sasa bado kuna gharama za malazi.
"Kwa kweli kukosekana kwa mdhamini kunazitesa timu nyingi hasa kwenye upande wa gharama, rai yangu wadau wasichoke kutupa sapoti kwani kama tutachelewa kwenda Mtwara tutawachosha wachezaji na tutashindwa kucheza kwenye ubora wetu," amesema Matola.
0 COMMENTS:
Post a Comment