May 22, 2019

Verified

MWENYEKITI wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kampuni ya Klabu ya Simba, Mohammed Dewji amesema timu ya Yanga inastahili pongezi kwa kuonyesha ushindani msimu huu licha ya Simba kutwaa ubingwa.

Simba jana ilitwaa ubingwa mbele ya Singida United baada ya kushinda mabao 2-0 uwanja wa Namfua na kuifanya ijikusanyie jumla ya pointi 91 ambazo haziwezi kufikiwa na timu nyingine.

Akizungumza na waandishi wa Habari kwenye Ofisi za MeTL Group zilizopo jengo la Golden Jubilee Towers Mo amesema kuwa kazi kubwa ambayo wameifanya Yanga msimu huu inaonesha ni namna gani walivyo na uwezo hivyo wanapaswa wajipange msimu ujao kufanya vizuri zaidi.

"Nawapongeza Yanga kwa hatua waliyofikia hivyo nina imani wameleta changamoto kubwa nawashauri wajipange upya kwa msimu ujao kwani ushindani utakuwa mkubwa.

"Pia kwa hatua ambayo wamefanya ya kuchagua viongozi ni nzuri na kubwa wanapaswa pongezi kwani waliochaguliwa nina imani wana uwezo mkubwa wa kusimamia kile ambacho kitaleta matokeo chanya," amesema Mo.


1 COMMENTS:

  1. Huyo ni kiongozi asiye na hasadi wala chuki na ndio mana akawa timu yake inmekuwa yake inateleza bila ya vikwazo na huu ni mfano WA kuigwa Kwa kila mstaarabu

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic