May 19, 2019


UONGOZI wa Singida United umesema kuwa kuelekea kwenye mchezo wao wa ligi dhidi ya Simba utakaochezwa Mei 22 uwanja wa Namfua wamejipanga kubeba pointi tatu.

Singida United ipo chini ya mchezaji wa zamani wa Simba Felix Minziro ikiwa nafasi ya tisa baada ya kucheza michezo 36 na ina pointi 45 kibindoni.

Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Singida United, Cales Katemana amesema mchezo huo ni zaidi ya fainali kutokana na umuhimu wa pointi tatu hasa wakiwa nyumbani.

"Tunatambua ubora wa Simba hilo halitupi taabu, tumejipanga kucheza kwa mtindo wa fainali tukiamini kwamba lazima mshindi apatikane.

"Morali kwa wachezaji ni kubwa na kla mmoja amepewa jukumu lake hivyo Jumanne si salama kwa Simba," amesema Katemana.

3 COMMENTS:

  1. Hawa singida kila mwaka tunawafunga hapo kwao lakini bado wanamdomo ngoja tuwasindilie ndanda kwanza bao 4,hawa singida tutawafanya tena daraja la kutangaza ubingwa.

    ReplyDelete
  2. Minziro aliwai chezea yanga sio simba. Mwandishi wewe aya tu. ��

    ReplyDelete
  3. Kwa nini timu zinapania Simba??... zikifungwa ooh Simba anabebwa hata sielewi huwa wanawasha na nini? Kwa umbumbu chukulia mfano mdogo tu kwa African Lyon hata ligi haijaisha ameshashuka daraja na kupania kote wakicheza na Simba.Kocha Aussem ameshasema hakuna mchezaji mwenye kiwango aliyemwona ktk timu zote 19 za ligi anayeweza kusajiliwa acheze Simba.Wachezaji jitambueni kuwa ligi sio timu moja tu mnayoshindana nayo.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic