May 19, 2019


UONGOZI wa Ndanda FC umesema kuwa wana imani ya kubeba pointi tatu mbele ya Simba kwa kuwa litakuwa daraja lao kubaki kwenye Ligi Kuu Msimu ujao.

Ndada FC ipo nafasi ya saba ikiwa imecheza michezo 35 na ina pointi 47 imebakiwa na michezo mitatu bado haina uhakika wa kubaki kwenye ligi msimu ujao endapo itapoteza michezo yake yote.

Akizungumza na Saleh Jembe, Katibu wa Ndanda FC, Seleman Kachele amesema ligi bado haijakamilika hivyo ni lazima wapambane kupata matokeo mbele ya Simba ili wasishuke daraja.

"Nafasi ya saba ambayo tupo si salama kwani kwa namna ambayo tumepishana pointi chache na wenzetu pamoja na michezo ambayo tumebakiwa nayo ni rahisi kufikiwa na imu nyingine.
"Hivyo mchezo wetu dhidi ya Simba ni lazima tupambane na tunazitaka pointi tatu za Simba ili tubaki kwenye ligi msimu ujao, mashabiki watupe sapoti kwani inawezekana kuitumia Simba kama daraja, wao wana uhakika wa kubaki kwenye ligi," alisema Kachele.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic