May 3, 2019


KOCHA Mkuu wa kikosi cha timu ya Taifa, Emmanuel Amunike amesema kuwa anahitaji mechi mbili ngumu kwa ajili ya kukiandaa kikosi chake kuelekea kwenye michuano ya Afcon itakayofanyika mwezi Juni, nchini Misri.

Tanzania imefuzu michuano hiyo baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya kikosi cha Uganda uliochezwa uwanja wa Taifa, Dar.

"Nahitaji michezo miwili migumu kwa ajili ya kuandaa kikosi changu kuelekea kwenye michuano ya Afcon ambayo tumeweza kufuzu, tupo tayari kupambana na kupata matokeo ila ni lazima tupate mechi mbili.

"Miaka 39 ni miaka mingi kwetu sasa ili tufanye vizuri ni lazima tucheze mechi mbili za kirafiki na timu ambazo zipo kwenye michuano hii tunayokwenda kushiriki," amesema Amunike.

Mchezo wa kwanza wa Stars nchini Misri utakuwa ni dhidi ya Senegal na mehi ake zitachezwa usiku na jana aliitangaza kikosi kitakachoingia kambini mwishoni mwa mwezi huu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic