May 7, 2019



RAIS  John Magufuli leo alikuwa miongoni mwa waliouaga mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Dkt. Reginald Mengi, kwenye Ukumbi wa Karimjee.

Magufuli ameungana na familia ya marehemu, marafiki, wafanyakazi wake, ndugu, jamaa na taifa kwa jumla kumwaga mtu ambaye aligusa watu wengi wakiwemo walemavu na watu wenye mahitaji maalum aliokuwa akiwasaidia enzi za uhai wake.

Mwili wa Mengi unaagwa leo Karimjee na kesho Jumatano, utasafirishwa kwenda kwao Machame ambako utazikwa Alhamisi.

Viongozi wengine waliokuwepo ni Makamu wa Rais, Samia Suluhu, Makamu wa Rais Mstaafu, Gharib Bilal, Waziri Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda, Spika Mstaafu, Anne Makinda, Jaji Mkuu, Prof. Ibrahim Juma, mawaziri, wakuu wa mikoa na wilaya, viongozi wa dini na viongozi wa serikali waliopo madarakani na wastaafu.

Mengi pia alikuwa ni mdau mkubwa wa michezo ambapo alikuwa ni shabiki wa Yanga na mlezi wa timu ya Tafa ya Vijana chini ya miaka 17, Serengeti Boys.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic