May 7, 2019



KOCHA Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera, amesema msimu huu hawana malengo ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu huu, licha ya kwamba hivi sasa bado wapo kileleni.

Yanga inaongoza Ligi Kuu Bara baada ya kucheza michezo 34 imejikusanyia pointi 80 huku mpinzani wao Simba akiwa amecheza michezo 30 na ana pointi 78 katika nafasi ya pili.

"Malengo yetu yalikuwa ni kuwa ndani ya 10 bora kwenye ligi na sio kutwaa ubingwa wa ligi kuu msimu huu, hivyo ilikuwa tangu awali na bado tunapambana," amesema Zahera.

Yanga imebakiwa na michezo minne kumaliza msimu huu huku Simba ikibakiwa nayo nane. Simba ikishinda kesho dhidi ya Coastal, itakaa kileleni.


4 COMMENTS:

  1. duh jamani Zuhura weee! unashindwa hata kukumbuka ulisema nini kuhusu mapinduzi cup, FA cup na ubingwa wakati ulipopeleka kikosi cha timu B Zanzibar

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hahahahhahahaha naona alisahau maana anachosema sasa hivi ni kwamba hawakuwa na mipango ya kuchukuwa ubingwa nadhani hii wangelisema mapema sisi ni washiriki tu na sio washindani bwana

      Delete
  2. Yanga wawe makini sana na huyu jamaa. Tayari hapo kwa kauli yake inaonyesha kuwa hiyo mipango ilipangwa na uongozi wote wa Yanga, kwamba malengo ya msimu huu ni kutafuta nafasi ya kuwemo kwenye kumi bora.

    Kama ndivyo, kwa Yanga hii ninayoijua mimi na kwa msemaji wao ninayemfahamu mimi (Ten), angesharopoka siku nyiiingiiii. Sasa iweje kauli hii iwe ya GHAFLA kiasi hiki!!!!!? Tena ni mara baada ya kufungwa na LIPULI na kutolewa kabisa katika kuwania kombe la FA?

    Hii nami naungana na Bwana TINO pale juu kuwa "SIZITAKI MBICHI HIZI". Halafu kauli hii anataka kuifanya iwe ndio silaha ya kuendelea kubaki YANGA.

    Hivi hajui kuwa kuna wenzake walitimuliwa wakati Yanga ikiongoza ligi lakini ikatokea mchezo mmoja tu ikafungwa au kutoa sare? Kocha anafungashiwa virago.

    Sasa alituambia na kutamba kuwa anataka amalize mechi zake zilizobaki kwa kushinda zoooteee (Mechi nne zimebaki). Tujiandae kupata kauli yake nyingine ya kujichanganya mara atakapopigwa na Biashara au Azam.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic