Kocha wa African Lyon Salvatory Edward, amesema kuwa michezo yao miwili iliyobaki watakaza ili kushinda licha ya kushuka Daraja msimu huu baada ya kucheza mechi 35 wakiwa na pointi 23.
Edward amesema kuwa kushuka Daraja haina maana kwamba wasipambane kwenye mechi zao kwani kanuni ya mpira hairuhusu kukata tamaa.
"Tunajua kwamba tayari hatupo kwenye ligi msimu ujao, ila kanuni za mpira zinatukataza kukata tamaa, hivyo michezo yetu miwili iliyobaki ni lazima tukusanye pointi tatu.
"Wachezaji wamekata tamaa kwa sasa na morali imeshuka kutokana na kutokuwa na cha kupoteza kwa sasa ndani ya ligi hilo tutalishughulikia," amesema.
Lyon jana waliongoza mchezo ndani ya dakika 81 uwanja wa Uhuru wakiwa mbele kwa mabao 2-0 yaliyofungwa na Murshid Bartoz dakika ya 21 na Awadhi Juma ila Mbeya City waliweka meza sawa dakika ya 82 kupitia kwa Victor Hangaya na Mohamed Kapera dk ya 90.

0 COMMENTS:
Post a Comment