May 3, 2019


Kikosi cha Yanga kinaondoka leo asubuhi kuelekea Mkoani Iringa ambapo siku ya Jumatatu Mei 6, 2019 kitacheza mchezo wa nusu fainali ya Azam Sports Federation Cup (ASFC) dhidi ya Wanapaluhengo Lipuli FC.

Yanga watakipiga na Lipuli, pambano litakalopigwa katika dimba la Samora kuanzia saa 10:00 Jioni.

Kuelekea mchezo huo, beki kisiki Kelvin Yondani ataambatana na timu kwani tayari amemaliza adhabu yake ya kukosa michezo mitatu.

Wakati Yondani akirejea, beki wa kushoto Gadiel Michael atakosekana kutokana na kuwa majeruhi baada ya kuumia katika mechi dhidi ya Azam.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic