UONGOZI wa Yanga umesema kuwa bado unatambua kwamba mshambuliaji wao tegemeo, Heritier Makambo ni mali yao na ataendelea kuitumikia klabu hiyo kwa kuwa ana mkataba wa mwaka mmoja.
Makambo mwenye mabao 16 kwa sasa kwenye ligi akiwa ni kinara wa kucheka na nyavu ndani ya Yanga imeripotiwa amesaini mkataba wa miaka mitatu katika timu ya Horoya AC inayoshiriki Ligi Kuu ya Guinea.
Mwenyekiti wa Yanga, Msindo Msolla amesema kuwa wana imani na mchezaji wao kwamba bado ni mali ya Yanga kutokana na kubakiwa na mkataba wa mwaka mmoja hivyo suala la kusaini bado halijafika mezani kwa Yanga.
"Makambo ni mali ya Yanga kwani bado ana mkataba hivyo suala la kuondoka lipo mikononi mwa Yanga wenyewe, mashabiki watulie kwani safari yake ilikuwa ni kwa ajili ya vipimo tu na sio kwenda kusaini mkataba," amesema Msolla
wabongo tunakwama wapi?hivi lini umesikia mchezaji anaenda kufanya vipimo vya afya kabla timu husika hazijakaa mezani kuelewana biashara?huu ni uzuzu
ReplyDeleteHuyu Mwenyekiti atashutukiwa kuwa ni mnyama hivi karibuni
ReplyDeleteYanga wamkomalie na Zahera vile vile kwani yeye ndie aliemtafutia dili.
ReplyDeleteMimi nilifikiri kuwa Uongozi Mpya umeingia mambo yanaenda kuwa na "afueni" pale Yanga imekuwa tofauti....kwani wachezaji tegemeo wanauzwa....mechi za zikiendelea, sherehe za Michango zinasitishwa na kuahirishwa, Kocha anakimbia/kwenda nje kuuza mchezaji, ahadi hewa na michakato na uongo kila kukicha....sasa sijui wana nia ipi? Wanayanga hebu jibuni haya maswali kabla chombo "akijaenda mrama"....msipumbazwe, Simba wanafurahia hii hali yenu.....kumekuwa na jitihada za kuwapotosha na kuwahadaa na kuwaridhisha wakati chombo hakiendi sawa.....msilale Yanga amkeni....."wanawapetipeti" kwa lugha za kuwalainisha mitandaoni....lakini ukweli ni kuwa hawana nia ya kuona Yanga inaimarika.....Fanyeni uchunguzi kwani kila maoni ya kupata wachezaji bora, benchi bora la ufundi na mambo mengine ya kuimarisha timu yanapotolewa utaona wanasema msajilini mchezaji fulani (wa bei ya chini kutoka hapa Tanzania tena mwenye kiwango cha kawaida, na ambae anatoka Simba au hata timu nyingine hali kiwango chake hata Simba hafai) ....Yanga kama mnataka maendeleo msikubali kuyumbishwa takeni na himizeni yaliyo juu hasa nikimaanisha usajili wa wachezaji level juu). Pili suala la kubadilisha mfumo wa uendeshaji lazima wawekezaji waanze kutafutwa ndani ya miezi 3....
ReplyDeleteKuna upotoshwaji na nia ya kutaka kuwatoa Yanga "nje ya reli/mstari"....wanachama na mashabiki amkeni sasa hivi mkihoji hivi vitu kabla vitu havijaharibika.....Uongozi huu lazima hukidhi matakwa ya wanayanga kuwa na timu bora....lakini dalili ya mvua ni mawingu.....nina maana kila mtu alifikiri Yanga itafanya usajili bora na kuanza kusuka kikosi bora haraka, lakini hali si hivyo....wanauza wachezaji tegemeo (makambo, nasikia tetesi fei toto yuko njiani pia) bila kureplace hii si dalili nzuri
Mwisho wa Maoni...