May 17, 2019



Emmanuel Okwi amesema kuwa bado mapambano yanaendelea mpaka dakika ya mwisho ili waweze kupata pointi tatu muhimu hivyo wameamua kwa pamoja kufanya maamuzi magumu kwa kushinda michezo inayofuata.


Okwi msimu huu ametupia jumla ya mabao 15 sawa na nahodha wake John Bocco amesema kuwa kwa sasa hesabu zao ni kuelekea mchezo wao wa Ndanda utakaochezwa Jumapili.

"Kwa sasa wachezaji wote akili zetu ni kuelekea mchezo wetu dhidi ya Ndanda, hivyo tutapambana kupata pointi tatu muhimu.

"Tumeteleza michezo yetu iliyopita hilo tunasahau na kuangalia kile kilicho mbele yetu, hivyo mashabiki waendelee kutupa sapoti," amesema Okwi.

Simba imecheza michezo 34 na imejikusanyia jumla ya pointi 85 ikiwa nafasi ya kwanza huku wapinzani wao Yanga wakiwa nafasi ya pili na wana pointi 83.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic