June 16, 2019


MODewji hataki kuona mchezaji ambaye bado anahitajika na Kocha Patrick Aussems pale Simba anaondoka ndiyo maana amevunja benki na kumpa nahodha msaidizi, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’ Sh mil 80 na mshahara wa kufuru.

Tshabalala alijiunga na Simba msimu wa 2014/15 akitokea Kagera Sugar. Mara ya mwisho wakati akiongeza mkataba Simba, Tshabalala alipewa dau la Sh mil 60. Chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya Simba, kimeliambia Championi Jumamosi kuwa, safari hii Simba imeboresha mahitaji ya nyota huyo na kumpa kiasi cha Sh mil 80 na mshahara wa Sh mil 4 kwa mwezi.

“Tshabalala kwa sasa mambo yake mazuri kwani ameongeza mkataba wa miaka miwili Simba na wamempa Sh mil 80 hivyo ataendelea kuwepo Msimbazi.

“Unajua awali meneja wake alikuwa anasikilizia kwanza ofa kutoka timu nyingine kwa kuwa mchezaji wake alichaguliwa timu ya taifa ambayo inacheza Afcon hivyo akawa anapiga hesabu kuwa wanaweza kupata ofa zingine kubwa.

“Hata hivyo siku chache kabla hawajasafiri kwenda Misri na timu ya taifa ndipo wakabadilisha maamuzi ya kusaini kabisa Simba.

“Pia wakahofia mchezaji anaweza akawa na mawazo wakati anacheza huku anafikiria mkataba mpya. Meneja wake, Kheri Chibakasi alisema:

“Tshabalala ni kweli ameongeza mkataba wa miaka miwili Simba hivyo sasa ataendelea kucheza Afcon bila presha kubwa na thamani yake kwa sasa ni ya juu kutokana na ubora wake.



“Simba wamemtimizia mahitaji yake kama ambavyo alikuwa anataka na kusema amesaini kwa bei gani na mshahara ni kiasi gani hilo litabaki kuwa siri ya mchezaji na klabu yake.”

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic