UONGOZI wa timu ya Manispaa ya Kinondoni, KMC umeamua kuendelea kuwapiga pini nyota wao wanaowahitaji ambapo leo tena wamemuongezea kandarasi mchezaji wao Cliff Buyoya.
Ofisa Habari wa KMC, Anwar Binde amesema kuwa mpango mkubwa uliopo kwa sasa ni kukisuka kikosi kipya cha ushindani.
"Mchezaji wetu Cliff Buyoya ataendelea kuitumikia KMC, tumemuongezea kandarasi ya miaka mitatu hivyo atadumu mpaka mwaka 2022," amesema.
Wachezaji wengine ambao tayari wameongeza mkataba ndani ya KMC ni pamoja na Salum Ilanfya na Hassan Kabunda wote pini zao ni miaka mitatu.
0 COMMENTS:
Post a Comment