June 2, 2019

LIVERPOOL imefuta machungu ya kukosa kombe la Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu uliopita mwaka 2017/18 ilipochapwa mabao 3-1 na Real Madrid baada ya jana kufanya hivyo mbele ya Tottenham Spurs kwa ushindi wa mabao 2-0 uwanja wa Wanda Metropolitano Jijini Madrid.

Hii ni mara ya sita kwa Liverpool kutwaa ubingwa baada ya kuanza miaka ya 1977,1978,1981,1984 na 2005.

 Mabao yao yalifungwa na Mohamed Salah ambaye alifunga bao lake la mapema dakika ya pili  kwa mkwaju wa penalti baada ya kiungo Moussa Sissoko kuunawa eneo la hatari mpira uliogongeshwa na fowadi Sadio Mane.

Muuaji wa pili Divock Orig dakika zake za usiku aliibuka na kupachika bao la pili dakika ya 88 baada ya kupiga shuti la chini lililozama nyavuni.

Hili linakuwa bao lake la nne kufunga dakika za lala salama kama ambavyo alifanya mbele ya Everton, Newcastle na Barcelona.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic