June 17, 2019


KOCHA wa timu ya Taifa ya  Senegal, Aliou Cisse amesema kuwa nyota wake Sadio Mane ataukosa mchezo wa kwanza wa ufunguzi wa michuano ya Afcon ambao watacheza dhidi ya Tanzania Juni 23 saa 2:00 usiku.

Mane ni staa wa Senegal ambaye anakipiga Liverpool ni miongoni mwa washambuliaji wakali kwani ana tuzo ya mfungaji bora wa Premier League akiwa ametupia jumla ya mabao 22, ataukosa mchezo huo kutokana na adhabu ya kadi mbili za njano.

Kadi hizo alizipata kwenye mchezo dhidi ya Guinea, Novemba mwaka jana na ule dhidi ya Madagascar Machi mwaka huu ambazo zilikuwa ni za kufuzu Afcon.

"Hata kama hatokuwepo bado tutabaki imara, Caf wameamua hivyo hatuwezi kupinga ila nina imani Mane atacheza mchezo wa pili dhidi ya Algeria na wa tatu dhidi ya Kenya ambao ni wa kuhitimisha hatua ya makundi," amesema,".

Stars ipo kundi C kwenye michuano ya Afcon inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi Juni 21 na mechi ya ufunguzi itapigwa kati ya wenyeji Misri na Zimbabwe.  

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic