June 17, 2019


MAMBO ni moto Simba! Hivyo ndivyo unavyoweza kusema baada ya uongozi wa timu hiyo kuingia msituni kutafuta bonge la Straika ambaye atakuwa ni moto wa kuotea mbali zaidi ya Mganda, Emmanuel Okwi pamoja na Mnyarwanda, Meddie Kagere.

Katika kufanikisha hilo taarifa ambazo Championi Jumatatu limezipata kutoka ndani ya timu hiyo zimedai kuwa uongozi huo chini ya bilionea Mohammed Dewji sasa umeamua kuwapa majukumu mazito baadhi ya mawakala wenye majina makubwa barani Afrika.

Mmoja wa viongozi Simba ambaye ameomba hifadhi ya jina lake amedai kuwa mawakala hao wametakiwa kuhakikisha wanampata mshambuliaji huyo ndani ya wiki mbili kuanzia sasa na thamani yake isizidi dola 150,000 (zaidi ya Sh 388 milioni).

“Lakini pia awe na rekodi nzuri katika michuano ya kimataifa siyo katika ligi ya kwao tu kama ambavyo ilikuwa kwa Mganda, Juma Balinya ambaye tuliamua kuachana naye kutokana na kutokuwa na rekodi ya kuvutia katika michuano ya kimataifa,” alisema kiongozi huyo na kuongeza kuwa:

“Mmoja wa mawakala waliopewa jukumu hilo ni Wakala wa Kagere, Patrick Gakumba ambaye tumekuwa tukifanya naye kazi vizuri.”

Alipoulizwa Gakumba kuhusiana na hilo alisema kuwa:“Ni kweli kabisa Simba wamenipatia jukumu la kuwaletea mshambuliaji wa nguvu mwenye CV kubwa katika michuano ya kimataifa.

“Kwa hiyo kwa kushirikiana na baadhi ya mawakala wengine pamoja na uongozi wa Simba hivi sasa nipo katika harakati kabambe ya kuhakikisha nashusha jembe la nguvu,” alisema Gakumba.

Alipotafutwa Mtendaji Mkuu wa Simba, Crescentius Magori, ili aweze kuzungumzia hilo hakupatikana kutokana na simu yake ya mkononi kuita tu bila ya kupokelewa.

10 COMMENTS:

  1. Sizitaki mbivu hizi! Juma Balinya mlimtaka sana Simba, mmezidiwa ujanja eti hana record za kimataifa..! Yanga kalamba dume acheni kebehi

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kwa akili ya kawaida ambayo haihitaji kudadafuliwa saaaana wala kuumiza kichwa. Huyo Balinyi na hatua waliyofikia simba kwenye michuano ya kimataifa unadhani kiwango chake kingeisaidia simba? Adam Salamba ametoka Lipuli kuja simba akifunga bao 10 lakini ameshindwa kuisaidia simba na hata kuleta upinzani kwa kina Kagere. Washambuliaji watatu pekee wametia kambani 50+ sasa anatakiwa mshambuliaji mwingine ambaye ataleta ushindani kwa hao watatu waliopo ambao na wenyewe kuna mmoja ama wawili wataondoka hivyo mchezaji kama Juma wala asingekuwa msaada kwa mikakati ya simba. Mfuatilie vyema utapata data zake kisha fikiria kwa marefu na mapana sio kuingiza ushabiki.

      Delete
    2. Mkude na Ajibu wako timu ya taifa!? Kucheza timu ya taiga ni nafasi na wakati!! Angalia no anayocheza huyo dogo na walioenda kule wanacheza wapi!? Kenya na Uganda zina wachezaji wengi wanaocheza nje kwahiyo sio rahisi kupata no kama bongo. Kagere ana record ipi kimataifa na umri wake!? Acheni wakati useme sio unaongea tu halafu unasema huongelei ushabiki

      Delete
    3. Kagere,mfungaji bora number 2 thailand pr lg 2014,goal 4 shirikisho 2017,mfungaji bora kenya misimu miwili,ana magoli 5 caf champions league 2018/2019.mfungaji bora tpl 2019.huwezi kumfananisha na mchezaji anaeibuka mfungaji bora kwa mara ya kwanza tena kwenye ligi mj.huyo ni kama ayee tu.

      Delete
  2. Angekuwa straika wa maana angekuwa timu ya taifa ya Uganda.The Cranes. Ni mchezaji wa kawaida sana sio hata level ya Makambo.

    ReplyDelete
  3. Yanga wamepigwa changa la macho kwa Balinya bora wangembakisha Amisi Tambwe nawapa ushauri wa wazi kabisa na wa kizalendo ingawa mimi ni mnyama.

    ReplyDelete
  4. fateni yenu ya Yanga hayawahusu !! yanga watumie akili ?? ninyi mnaotumia akili na
    mshambuliaji gani wa kimataifa mtakaemsajili kwa pesa ndogo kama hizo USD.150,000 ??
    mbona majiulizi na kutumia akili hapo ??

    ReplyDelete
    Replies
    1. Balinya a.k.a Aiiyee wa uganda aliyesajiliwa kwa 50 mil tutasemaje?

      Delete
  5. Kuwa mshabiki Wa yanga cjui uelewa unatoka au huwa wankuwaje hiv simba kufanya usajili Wa level ya lipuli kweli? Yaani Hugo juma aje simba kama straika? Si bora umchukuwe makambo?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic