STRAIKA wa Mwadui Salim Aiyee ameshindwa kwenda nchini Sweden baada ya Pasipoti yake kutokukamilika kwa wakati.
Aiyee alitakiwa kusafiri Juni 15, kwenda nchini Sweden kwa ajili ya kwenda kufanya majaribio katika moja kati ya timu inayoshiriki ligi kuu ya huko ambayo hataki kuiweka hadharani.
Aiyee aliliambia Championi Jumatatu kuwa alitakiwa kusafiri Jumamosi lakini alishindwa kutokana na Pasipoti yake kutokukamilika ambapo alisema kuwa itakamilika Jumatatu ndipo apange tena safari.
“Nimeshindwa kusafiri kwa kuwa Pasipoti yangu haijakamilika hivyo wameniambia kuwa leo Jumatatu itakuwa tayari ishakamilika.
Pia aliongeza kuwa anatakiwa awahi mapema iwezekanavyo kwa kuwa Juni 20 kuna mechi anatakiwa acheze kama sehemu ya majaribio ya timu hiyo.
0 COMMENTS:
Post a Comment